Waziri 'Mwigulu Nchemba' Aliposimama Kufafanua Kuhusu Vitambulisho!
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dr. Mwigulu Nchemba amewataka watanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa kwani si zoezi la hiari ni lazima kwa mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi ili kutambuliwa.
Waziri Nchemba, amesema hayo alipokuwa akizindua zoezi la kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa na kugawa vitambulisho katika mkoa wa Tabora na kukagua zoezi hilo linavyoendelea kwa sasa.
Waziri Mwigulu amewataka wananchi waache mazoea ya kutafuta kutambuliwa mpaka wanapokuwa na shida hasa za kutaka hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa Tanzania .
"Zoezi hili ni bure kujiandikisha na kupata kitambulisho pasitokee kiongozi yeyote wa wilaya na vijiji kuchangisha fedha wananchi ili wapate fomuza kujiandikisha na wala zoezi hili lisiunganishwe na siasa."alisema Dr.Mwigulu
Naye Kaimu Mkurugenzi mkuu wa vitambulisho vya Taifa Andrew Masawe amesema zoezi la kuandikisha wananchi linatakiwa kuisha ifikapo mwezi December 2018 na mpaka sasa mikoa 19 imeshaanza kuandikisha wananchi kupata kitambukisho cha utambuzi, huku mkoa wa Mala, Arusha , Mwanza Simiyu na Ruvuma ikifanya vizuri katika uandikishaji wananchi.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Tabora ambaye ni mkuu wa wilaya ya Tabora Queen Mlozi amesema wao kama mkoa wamejipanga kila wilaya wataendesha zoezi hilo kwa kushirikiana na taasisi zingine kama uhamiaji kuwatambua raia halali wa Tanzanaia na kila mwananchi andikishwe.
Subscribe muda huu www.youtube.com/user/uwazi1
Install #GlobalPublishersApp
Android: [ Ссылка ]
iOS: [ Ссылка ]
Subscribe [ Ссылка ]
FACEBOOK: [ Ссылка ]... TWITTER: [ Ссылка ] Visit [ Ссылка ], Subscribe [ Ссылка ] Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… [ Ссылка ] [ Ссылка ] [ Ссылка ] WEBSITE: [ Ссылка ] FACEBOOK: [ Ссылка ]... TWITTER: [ Ссылка ] INSTAGRAM: [ Ссылка ]..
Ещё видео!