Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amembana Mkandarasi M/s China Railway 15 Bureau Group Corporation akimtaka aeleze sababu za kusuasua kwa ujenzi wa sehemu ya tatu ya Barabara ya Tungamaa- Mkwaja -Mkange wilayani Pangani mkoani Tanga yenye urefu wa kilomita95.2. yenye thamani ya Sh 111.55 bilioni.
Njia hiyo ni sehemu ya barabara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na ipo kwenye ushoroba wa Pwani ya Afrika Mashariki unaoanzia Malindi -Mombasa Lunga Lunga Kenya na Horohoro na Tanga-Pangani - Bagamoyo Tanzania wenye urefu wa jumla ya kilometa 454.
Waziri Ulega amembana mkandarasi leo Alhamisi Januari 2, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo miradi ya Barabara ya Tanga- Pangani na daraja la Pangani.Katika ziara hiyo aliambatana na viongozi waandamizi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), akiwa na Mtendaji Mkuu, Mohamed Besta.
Moja ya sababu alizitoa mkandarasi huyo ni changamoto zinazokwamisha ujenzi huo ni mvua zinazonyesha mara kwa mara “Ni kweli hatujafanya vizuri kwa sababu ya mvua nyingi kunyesha, lakini upatikanaji wa malighafi hasa kipande cha pili cha tatu cha barabara hali inayosababisha ujenzi kwenda kidogo kidogo.”
Hata hivyo, Waziri Ulega hakukubaliana na suala hilo, kwa mujibu wa Ulega, ameangalia mwenendo wa mtiririko wa fedha kwenda kwa mkandarasi huyo, amebaini haidai fedha nyingi Serikali hadi kushindwa kutimiza majukumu yake hayo kwa wakati.
Video na Ammari Masimba
Ещё видео!