Zaporizhzhia. Kombora lililorushwa na vikosi vya Russia limesababisha vifo vya watu takriban 13 huku zaidi ya 63 wakijeruhiwa eneo la Zaporizhizhia Kusini Mashariki mwa Ukraine.
Taarifa ya kutekelezwa kwa shambulizi hilo imetolewa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu nchini Ukraine, ambayo imesema Russia ilifanya shambulizi hilo usiku wa kuamkia leo Alhamisi Januari 9,2024.
Kwa mujibu wa ofisi hiyo, shambulizi la Russia lilisababisha miili kutapakaa barabarani yanapopita magari ya Umma huku sehemu ya barabara hiyo ikiharibiwa vibaya.
Kwa mujibu wa Shirika la Reuters, ofisi hiyo imesema watu 63 walikuwa wameshaokolewa kutoka kwenye jengo la makazi lililolengwa na shambulizi hilo huku shughuli ya kuwanasua waliosalia ndani ya jengo hilo ikiendelea.
Jengo hilo lenye ghorofa zaidi ya tano lililengwa na kombora hilo sambamba na jengo linalotumika kama kiwanda huku kifusi chake kikitajwa kuleta madhara kwenye magari yaliyokuwa yanapita karibu na eneo lilipofanyika shambulizi hilo.
Wakati watoa huduma ya dharura wakiendelea kunasua watu, moto na moshi mkubwa unaonekana ukifuka kuzunguka eneo ambalo limefanyika shambulizi hilo.
Gavana wa Mkoa wa Zaporizhizhia nchini humo, Ivan Fedorov amesema vikosi vya Russia vinatumia mabomu kulenga maeneo ya makazi.
Watu wanne kati ya 63 waliojeruhiwa wamekimbizaa hospitalini huku hali zao zikionekana kuwa mahtuti huku akitangaza Alhamisi kuwa siku ya maonlmbolezo ya watu waliofariki katika shambulizi hilo.
"Hakuna kitu kibaya kama kurusha kombora katika Jiji ambalo unajua kabisa kwamba wanaokaa pale ni raia,” aliandika Rais Volodymyr Zelenkyy kwenye Akaunti yake ya X (zamani Twitter), huku akiyatakama mataifa ya magharibi kuamka na kuishughulikia Ukraine.
Mbali na shambulizi katika jengo hilo,
Fedorov amesema kuna mashambulizi mengine yaliyofanywa na vikosi vya Russia hususan ni katika Mji wa Stepnohirsk, Kusini mwa Zaporizhzhia, na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo.
Katika shambulizi hilo, watu wawili waliokuwa wamenasa chini ya kifusi walitolewa ndani ya jengo wakiwa hai chini ya vifusi.
Imeandaliwa na Mgongo Kaitira
Ещё видео!