Mtazamaji wa Bongo News TV leo Oktoba 28, 2024 majira ya mchana WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ametembelea mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu na kujionea mwenyewe ukarabati uliofanywa na kikosi cha wahandishi wa Dawasa na wizara, baada ya kutokea kwa hitilafu katika moja ya mitambo kiasi cha kuathiri uzalishaji wa maji safi na salama.
Aweso amewahakikishia wakazi wa Dar es Salaam na Pwani kuwepo na upatikanaji wa maji safi na salama katika mikoa hiyo kwani changamoto ya hitilafu ya mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu juu tayari imerekebishwa.
#sports #entertainment #BONGONEWSTV Usisahau ku-subscribe channel hii kwa taarifa nyingi zaidi na pia tembelea mitandao yetu ya kijamii Instagram @bongonewstz twitter @bongonewstz na Facebook @bongonewstz
Ещё видео!