Mkutano unaohusu masuala ya Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) umefanyika Maputo, Msumbiji chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Msumbiji Fellipe Nyusi.
Marais kutoka Nchi tano ikiwemo Afrika Kusini, Botswana, Malawi na Mwenyeji Msumbiji wamehudhuria ambapo kwa upande wa Tanzania Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi amemuwakilisha Rais Samia Suluhu katika mkutano huo.
Nyusi amezishukuru Nchi Wanachama na kuwaomba kuendelea kuzidisha ushirikiano katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarishwa zaidi sio tu katika eneo la Cabo Delgado lililokumbwa na tishio la ugaidi bali kwenye Jumuiya yote.
Mapema Mtendaji wa SADC Dkt. Stargomena Tax alisema suala la ugaidi ni gumu na haliwezi likaachiliwa kwa Nchi moja pekee.
Ещё видео!