Rais William Ruto leo amependekeza watu 22 kwa uteuzi katika baraza lake la mawaziri. Miongoni mwa aliowapendekeza kwa uteuzi ni aliyekuwa naibu spika katika bunge la seneti Prof. Kithure Kindiki, seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen, mbunge wa Garissa Mjini Aden Duale na mwenzake wa Kandara Alice Wahome. Rais Ruto pia akionekana kuwazawadi wandani wake wakuu katika muungano wa kenya kwanza. Huyu hapa Francis Gachuri na orodha kamili ya baraza la mawaziri.
Ещё видео!