LEO TENA
ANHA LEO TENA HATA HAYA HUNA UTAZIDI KUSONONA
Nimepokea salamu hizo ulonitumia kuwa sasa unahamu mapenzi kuyarudia
Pendo nilokukirimu kwa dhati na safi nia nawe usiliheshimu mara ukalisusia
Wallah sina wazimu wewe kukurejeshea mempa mwenye nidhamu roho ilomtulia
Kuna jambo maktubu hilo shoti ufahamu ulinifikiri dubu sina akili timamu
Nimepata mahbobu anaenitia damu yeye ndo tiba ya hubu mwenye mapenzi matamu
Wataka tena zabibu umekumbuka utamu hata kama umetubu kukupa tena kharamu
Lau hukunikashifu pengine ningekubali mola kakutoa khofu hisani hukuzijali
Mepata muadilifu twapendana kweli kweli kwako nimestaafu kurudi mustahili
Mtu aso inswafu kheri kuwa nae mbali usilete tasnifu kuchezewa skubali
Huyo nilonae sasa anipendeza kwa mengi raha na kila anasa ndo ukaona sikongi
Sikurejei kabisa nilipovunja sijengi menitosha vyako visa na kujua kwako kwingi
Ulidhani ntakosa hujua mko wengi shika kama huna pesa ukaniroge giningi
#lyricvideo #zanzibarorchestra #zanziar orchestra #oldisgold #vyakaledhahabu
Ещё видео!