Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imeonya kwamba huenda uchaguzi ukaahirishwa katika sehemu 31 zinazokumbwa na mizozo ya uteuzi mahakamani. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati ametoa wito kwa idara ya mahakama kukamilisha kesi hizo na kutoa maamuzi kwani kuendelea kucheleweshwa kwa uamuzi wa mahakama kunaathiri maandalizi ya uchaguzi hasa uchapishaji karatasi za kura. Chebukati alikuwa akizungumza wakati wa kongamano la kitaifa kuhusu uchaguzi wenye amani lililoandaliwa na tume ya uwiano na mshikamano wa kitaifa NCIC ambako vyama vya kisiasa na wawaniaji urais wanne walitia saini mkataba wa uongozi na amani kama ahadi ya kuendeleza kampeni zao kwa amani.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: [ Ссылка ]
Follow us on Twitter: [ Ссылка ]
Find us on Facebook: [ Ссылка ]
Check our website: [ Ссылка ]
#ELECTIONS #NCIC #IEBC
Ещё видео!