Available on all Platforms: [ Ссылка ]
Download or listen online: [ Ссылка ]
Performers: Holy Spirit Catholic Choir Langas
Producer: Verony Productions Ltd.
Composer: Ochien'g Odongo
Copyright ©Verony Productions Ltd.
Nimeahidi Yesu - kukutumikia
Wewe u Bwana wangu - u rafiki pia
Sitaogopa vita - wewe ndiwe mweza
Sitaiacha njia - ukiniongoza
Imbeni aleluya, aleluya, imbeni
Shangwe kwa Bwana Yesu, ndiye mweza wetu
Dunia i karibu - Bwana siniache
Na mengi majaribu - yako pande zote
Siku zote adui - ni ndani na nje
Bwana Yesu nivute - karibu na wewe
Nikusikie wewe Bwana - nenda nami Bwana
Kelele za dunia - ndizo nyingi sana
Nena kunihimiza - au kunionya
Nena nikusikie - mwenye kuniponya
Umewapa ahadi - wakufuatao
Kwenda uliko wewe - wawe huko nao
Nami nimeahidi - kukutumikia
Nipe neema Bwana - ya kukwandamia
Hatua zako Bwana - na nizikanyage
Wewe u mwenye nguvu - mimi ni mnyonge
Niongoze nivute - nishike daima
Mwishoni niwasili - mbinguni salama
Ещё видео!