Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya DCEA imekamata zaidi ya Kilo 3,180 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine katika Mikoa ya Dar es Salaam na Iringa ikiwa ni idadi kubwa zaidi kukamatwa tangu shughuli za udhibiti zianze nchini.
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya DCEA ARETAS LYIMO amesema, dawa hizo zilizokamatwa Kigamboni, Kinondoni, Ubungo na Mkoani Iringa kiwango kikubwa zaidi kihistoria kuwahi kukamatwa tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya nchini.
= = =
![](https://s2.save4k.org/pic/z0qhyxcOgv0/maxresdefault.jpg)