Imebainika kwamba magaidi waliotekeleza uhalifu hapa Jijini Nairobi katika jumba la Westgate walikuwa na muda wa kuzuru benki moja ya Queensway Barclays na kutoa pesa ambazo wangetumia kununua gari aina ya Mitsubishi Lancer ambalo lilitumika kutekeleza uhalifu huo aidha kikosi cha polisi cha kupambana na ugaidi kibaini kwamba gari hilo lilikuwa chini ya jina la mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kushirikiana na magaidi hao. Kando na hayo maafisa wa usalama huko Mombasa wamewakamata washukiwa watatu wa ugaidi. Mwanahabari wetu Philip Murutu ana maelezo zaidi.
Ещё видео!