Yohana 6:56
[56]Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.
Yule mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu kwa muda wa miaka 12 aliposhika tu pindo la vazi la Yesu alipokea uponyaji wake palepale,hii inatuonesha kwamba hauwezi ukakaa au ukakutana na Yesu na ukabaki kama ulivyo.Mungu akiwepo kwenye eneo fulani vitu hubadilika.
Hapo ni Yesu aliyekuwa nje,lakini sisi ametupa nafasi kubwa zaidi ya kumgusa,ametupa nafasi ya kula mwili wake na damu yake,ametupa nafasi ya Yeye kukaa ndani yetu.Ni zawadi kubwa sana maana anapoingia ndani yetu hubadili na kuondoa kila ambacho sio pando lake kwetu na huleta kila ambacho ni mapenzi yake kwenye maisha yetu.
Katika ibada hii tulipata neema ya kushiriki mwili na damu yake na tumeshuhudia akifungua watu wengi kutoka katika vifungo vya nguvu za giza kwa ukubwa sana.
Umbali sio kigezo,kama Mungu alivyofanya kwa hawa akafanye na kwako pia.
UNAWEZA WASILIANA NASI AU KUTUMA SADAKA YAKO KWA NAMBA HII : 0657 173 322
Unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii
Like our Facebook: [ Ссылка ]...
Follow our Instagram: [ Ссылка ]...
Subscribe our YouTube: [ Ссылка ]...
Also Subscribe Roc worshippers youtube channel:[ Ссылка ]
Ещё видео!