Maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi yameshuka katika Mkoa wa Njombe kutoka asilimia 14 na kufika Asilimia 11.4 wakati katika mikoa ya Tanga na Dodoma maambukizi hayo yakipanda kwa asilimia 2.6.
Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati wa Maadhimisho ya Miaka 15 tangu kuanzishwa kwa mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Katika maadhimisho hayo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi alisema atazindua Kampeni ya Wanaume Kupima VVU Jijini Dodoma, Juni 19.
Ещё видео!