Kamati ya masuala ya fedha katika bunge la kaunti ya Kajiado imehimiza tume ya maadili na vita dhidi ya ufisadi-EACC pamoja na idara ya upelelezi wa jinai kuchunguza madai ya ufujaji wa pesa za umma katika kaunti hiyo. Wakati wa warsha ya umma katika eneo la Ngong, kamati hiyo ya fedha ilielezea kutoridhika kwake kutokana na kutokamilishwa kwa miradi huku malipo yakitolewa kwa wana-kandarasi bandia kwa miradi ambayo haijakamilika. Wanachama wa kamati hiyo wamemtaka gavana wa Kajiado, Joseph Ole Lenku kukadiria upya miradi yote iliyofadhiliwa na serikali yake huku wakihimiza uwajibikaji na kushtakiwa kwa watuhumiwa wa ulaghai huo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: [ Ссылка ]
Follow us on Twitter: [ Ссылка ]
Find us on Facebook: [ Ссылка ]
Check our website: [ Ссылка ]
#kbcchannel1 #news #kbclive
Ещё видео!