Bwana Yesu asifiwe wadada wazuri,
Leo tunamshukuru Mungu na tunaendelea na masomo yetu kwa wasichana wa MY SEASON na groups za VYUO VIKUU..
Kuna watu wengi ambao wako kwenye mahusiano au wanakaribia kuingia na hawajui kama hao vijana wana "intensions" sahihi au la,
Wanawapenda ukweli au la..
Leo nataka tujifunze sawa na kisa cha AMNONI NA TAMARI,
Neno linasema
“Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya umbu lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lo lote.”
2 Sam 13:2 SUV
Yani alimpenda mpaka Akaugua...
Lakini neno pia linasema;
“Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako.”
2 Sam 13:15 SUV
Kisha neno linasema akamchukia sana
Huyu ni mwanaume huyo huyo mmoja,
Nini kinaendelea hapa kwa huyu kaka
Ukweli na uwongo kwa mwanaume unavijuaje?kama hana malengo unajuaje??
Tujifunze somo hili na Roho Mtakatifu atusaidie kufanya maamuzi sahihi kwa jina la Yesu..
MWAKA HUU UTAMALIZA NA MAHUSIANO YAKO SAHIHI KWA JINA LA YESU..
Min Mocky
Ещё видео!