Mabingwa wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara, wamehitimisha msimu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, matokeo yanayowafanya wamalize msimu bila kupoteza mchezo wowote.
Goli la kwanza kwenye mchezo huu uliochezwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, limefungwa na Denis Nkane, likiwa ni goli lake la kwanza kabisa kwenye ligi tangu ajiunga na Yanga.
Katika mchezo huu pia, Fiston Mayele alitikisa nyavu dakika za majeruhi, lakini ilikuwa ni 'off-side'.
Ещё видео!