Vita ya kukabiliana na dawa za kulevya zinazoathiri nguvu kazi ya Taifa hasa vijana, imeendelea kushika kasi na sasa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiania na vyombo vingine vya usalama, imekamata dawa za kulevya aina ya methamphetamine na heroin zenye uzito wa kilo 673.2.
Kati ya dawa hizo, kilo 448.3 ziliwahusisha raia wanane wa Pakistani waliokamatwa katika Bahari ya Hindi, zikiwa zimefichwa ndani ya jahazi lililosajiliwa nchini Pakistani kwa namba B.F.D 16548.
Pia, kilo 224.9 zilikamatwa kwenye fukwe za Bahari ya Hindi katika Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa leo, Alhamisi Januari 9, 2025 na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tathmini ya dawa kulevya zilizokamatwa kwa kipindi cha mwaka 2024.
Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi
(Imeandikwa na Hadija Jumanne)
Ещё видео!