Utetezi wa WEMA Mahakamani Leo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam,imeaza kusikiliza utetezi wa mshtakiwa ambaye ni muigizaji, Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa na Matrida Abas, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaona wana kesi ya kujibu katika mashtaka yanayowakabili ya kutumia dawa za kulevya.
Katika kesi ya msingi, Wema anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. ambapo wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa kosa moja la kukutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya.
Watuhumiwahao wameanza kujitetea mbele ya Hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na Washtakiwa hao wanatetewa na wakili Alberto Msando ambaye alikuwa akiwaogoza katika kuwauliza maswali juu ya nini wanafahamu kuhusiana na tukio hilo kuanzia Februali 4, 2017 hadi walipofikishwa polisi.
Inadaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda kosa hilo Februari 4 mwaka huu, nyumbani kwao Kunduchi Ununio , Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.
Install GlobalPublishersApp Android: [ Ссылка ] iOS: [ Ссылка ] Subscribe [ Ссылка ] FACEBOOK: [ Ссылка ]... TWITTER: [ Ссылка ] Visit [ Ссылка ], Subscribe [ Ссылка ]
Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… [ Ссылка ] [ Ссылка ] [ Ссылка ] WEBSITE: [ Ссылка ] FACEBOOK: [ Ссылка ]...
TWITTER: [ Ссылка ] INSTAGRAM: [ Ссылка ]..
Ещё видео!